Saturday, July 1, 2017

Sina hofu na ujio wa Okwi - Kessy

Beki wa Yanga Hassan Kessy amesema ujio wa mshambuliaji raia wa Uganda wa Klabu ya Simba Emmanuel Okwi haumtishi.

 Kessy amesema siku zote anapenda akabane na mchezaji tegemeo wa timu pinzani kwa ajili ya kumpa ushindani ili aone upungufu wake ili aweze kuufanyia kazi.
"Naheshimu uwezo alionao Okwi lakini siyo kumuogopa na katika kuthibitisha hilo, nitaanza kumuonyesha tutakapokutana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii," .
"Mimi na Okwi tunajuana kutokana na kuwahi kukutana katika mechi mbalimbali mimi nikiwa nachezea Mtibwa Sugar na yeye akicheza Simba, " amesema.
Kessy amesema anaamini ushindani utakuwa wa hali ya juu kutokana na kila klabu kusajili kutokana na mapungufu yaliyotokea katika msimu uliopita lakini yeye kwa upande wake anaendelea kujipanga ili kuhakikisha anafanya vizuri katika msimu ujao.


    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments