Friday, July 21, 2017

Man United waichakaza Man City bila huruma

Klabu ya soka ya Manchester United imeendeleza ushindi katika mechi zake za kirafiki huko nchini Marekani

United ambao walikuwa wakicheza na majirani zao Manchester City asubuhi hii katika mechi ya kirafiki ya kombe la International Champions Cup 2017 mjini Houston, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Magoli hayo ya Man United yaliyofungwa  na Romelu Lukaku dakika ya 37 na Marcus Rashford dakika ya 39.



    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments