Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai
amewaonya wabunge wanaochafua hali ya hewa kwa kauli za matusi na maudhi
bungeni waache mara moja kwani vitendo
hivyo ni vibaya kwa
wapiga kura wao huku akiwashangaa kuwa huenda wakawa na matatizo yao
binafsi yanayowasumbua.
Huku Ndugai akisema kuwa
“Unajua sisi tunaokaa hapa mezani hatuchangii kama nyinyi, kazi yetu ni kuwapa nafasi mseme, wakati mwingine zinatoka shutuma ambazo hatuna nafasi ya kubishana au kulumbana lakini wakati mwingine ni vizuri kutumia fursa hizi kusafisha baadhi ya mambo. Binadamu ni lazima uwe na staha ile ndogo tu kuwaheshimu binadamu wenzako,” akiwa amesisitiza kuwa
“Katika bunge letu kinacholeta matatizo humu ndani ni tabia na lugha, tukirekebisha hayo mawili tutaenda vizuri tu lakini najua kundi hili ni kubwa hatuwezi kuwa wote tupo sawa, nitaendelea kulisemea lakini pale kwenye ulazima tutachukua hatua,”
Hata hivyo Mh Ndugai amewaonya wabunge wanaochafua hali ya hewa bungeni kwa lugha chafu waache vitendo hivyo kwani hao ndiyo wanaoudhi kwa kauli zao za kusema bunge ni dhaifa huku akisisitiza kuwa wabunge aliowapa adhabu bado adhabu yao iko pale pale ya kukaa nje ya bunge kwa mwaka mmoja.
No comments:
Write comments