Licha ya ukaribu wao kuchukuliwa kama kiki, msanii Harmorapa amezidi
kusisitiza yupo katika mahusiano ya kimapenzi na video vixen Amber Lulu
licha ya mrembo huyo kuwahi kukanusha hilo
Harmorapa ambaye amekuwa akivutia watu wengi kwa vituko vyake, ameiambia Boys Boys ya TV1 kuwa yeye kama kijana wa kiume ni lazima awepo katika mahusiano.
“Unajua siku zote kama ni mwanaume, halafu mwanaume rijali ni lazima uwe kwenye mahusiano ya kimapenzi, kwa hiyo mimi nina mpenzi, kuoa bado hata mtoto sina. Kwa sasa ni mtu famous, nilishamtaja ili kuna wengine hawamfahamu ni Amber Lulu,” amesema Harmorapa.
No comments:
Write comments