Watu 25 wamefariki dunia na wengine takriban 20 wamejeruhiwa kutokana na
moto mkubwa uliozuka katika msitu uliopo katikati mwa nchi ya Ureno.
Naye waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, João Gomes amewaambia waandishi habari kuwa watu 16 wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, pale walipokabiliwa na moto huo mkubwa katika Wilaya ya Pedrógão Grande katika barabara inayounganisha miji ya Figueiro dos Vinhos na Castanheira de Pera.
Wakati huo huo waziri mkuu António Luís Santos da Costa, amesema hilo ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
No comments:
Write comments