Tuesday, June 13, 2017

Diamond asema Wema anamchango mkubwa sana kwenye Chibu Perfume

Msanii wa muziki Naseeb Abdul al-maarufu Diamond Platnumz ameamua kufunguka kwa kusema ukweli  juu ya mchango wa aliyekuwa mpenzi wake Wema Sepetu kuhusiana na  perfume yake ya "Chibu Perfume"

Huku Diamond akisema mara nyingi tu huwa anakutana  na Wema sepetu tofauti na  kushauriana juu ya mambo ya biashara

“Mimi na Wema labda watu hawajui sisi tunaongea sana wakati mwingine tunakutana tu sana lakini sio kwenye media. Tushakuwa kila mtu ana mahusiano yake tofauti yeye ana familia yake hata ukiangalia katika Perfume yangu lile neno THE SCENT YOU DESERVE alilitoa Wema” alisema Diamond.
Muimbaji huyo kwasasa yupo kwenye mahusiano ya Zari na tayari wamefanikiwa kupata watoto wawili.

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments