Sunday, June 18, 2017

Majeruhi wa Lucky Vicent kurejea nchini Agosti

Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha, walionusurika katika ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva  huenda wakarejea nchini baada ya miezi miwili.


Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ametoa taarifa hiyo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram katika mahojiano na waandishi wa habari,akisema kuwa kuna matumaini ya  watoto wote watatu kuweza kutembea na kuna uwezekano  wa kurejea Tanzania baada ya miezi miwili ijayo.

Huku mtoto Doreen anatarajiwa  kuhamishwa Madonna Center katika mji wa Lincoln, Jimbo la Nebraska kwa "Therapy" maalumu ya uti wa Mgongo wiki ijayo. Wanasema katika wote watatu Doreen ni muujiza mkubwa zaidi.




    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments