Msanii Baraka The Prince amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hana
tofauti yoyote na Alikiba na kudai kuwa watu wa mitandaoni ndiyo
wamekuwa chanzo cha kusambaza maneno hayo kuonyesha yeye ana tofauti na
Alikiba.
Baraka The Prince amedai kuwa yeye hawezi kugombana na Alikiba na wala
hategemei kuja kumkosea kwa kuwa ni moja kati ya watu ambao wanampenda
sana yeye pamoja na sanaa yake.
Mbali na hilo Baraka The Prince amesema
kuwa mkali huyo wa Aje hivi sasa yupo kwenye maandalizi ya kuachia kazi
yake mpya baada ya Aje kusumbua zaidi ya mwaka mzima.
Alikiba na Baraka The Prince licha ya
kuwa chini la label moja ya RockStar4000 wasanii hao pia waliachia kazi
ya pamoja ambayo inafahamika kama 'Nisamehe' .
No comments:
Write comments