Nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani Beyonce amejifungua mapacha kulingana na vyombo vya habari nchini Marekani.
Vyombo
vya habari vya Entertainment Weekely, Us Weekly na People Magazine
vimethibitisha habari hizo lakini tarehe ya kuzaliwa na jinsia ya watoto
haijajulikana.Beyonce ambaye ni mkewe mwanamuziki wa mtindo wa Rap Jay Z alitangaza kwamba ni mjamzito katika picha ya Istangram mnamo mwezi Februari ambapo ni picha iliopendwa mno katika historia ya mtandao huo.
Hakujakuwa na tangazo rasmi kuhusu kujifungua huko kutoka kwa Beyonce na Jay Z mwenyewe.
No comments:
Write comments