Mshambuliaji wa zamani wa kikosi cha Simba Emmanuel Okwi ambaye jana
amerejea rasmi katika kikosi hicho baada ya kusaini mkataba wa
kuitumikia Simba amefunguka na kusema amekuja kupambana kuhakikisha kuwa
Simba inapata ubingwa na kufanya vizuri.
Okwi anasema amefurahi sana kurudi katika timu yake hiyo ya zamani ikiwa chini ya viongozi wapya ambao ambao wanaonekana na njaa ya timu yao kufanya vizuri zaidi hivyo ameahidi kushirikiana nao na kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema.
No comments:
Write comments