Monday, June 26, 2017

Mwigulu Nchemba:wanaotaka ushoga watafute nchi ya kwenda

Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida, Mwigulu Nchemba amefunguka na kuwataka watu wanaotaka haki za ushoga watafute nchi ya kwenda ambayo isatoa haki hiyo lakini si Tanzania.



Mwigulu Nchemba anasema kama kuna taasisi yoyote imesajilikuwa nchini na inafanya kampeni za haki za ushoga basi atazifutia usajili huo na watu wake kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

"Wanaotaka haki za ushoga watafute tu nchi yao nyingine ambayo inaruhusu mambo hayo wakakae huko, kama ni taasisi imesajiliwa kwenye nchi yetu tukaigundua inafanya kampeni ya haki hizo na bahati nzuri zinasajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani nitazifutia usajili wao, na kama ni raia wa Tanzania anaendesha kampeni hizo tutamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria, na kama si raia amekuja kwenye nchi yetu kuja kuendesha haki hizo tutampa amri ya kuondoka ndani ya nchi yetu hatapata fursa hata ya kuchomoa chaji ya simu kwenye soketi ya umeme" alisisitiza Mwigulu Nchemba .

Mbali na hilo Mwigulu Nchemba alipigia msumali kauli ya Rais dhidi ya wanafunzi ambao watapata ujauzito wakiwa shuleni na kusema watu wanaopinga jambo hilo wasitumie nguvu kubwa kupinga bali wajenge shule zao wao watoe hiyo haki ya kusomesha wanafunzi wajawazito au wale ambao tayari wamejifungua na siyo kulazimisha serikali ya Magufuli kufanya hayo

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments