Monday, June 26, 2017

Marufuku kusafirisha chakula nje - Majaliwa

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa apiga marufuku usafirishaji wa chakula nje ya nchi bila kibali na kuwataka wafanyabiashara kuuza chakula kwenye maeneo yenye uhaba nchini.



Mhe. Majaliwa ametoa agizo hilo leo, wakati akihutubia Baraza la Iddi katika msikiti wa Masjid Riyadh mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kuwa kuna maeneo ambayo wananchi hawakupata chakula vizuri kutokana na uhaba wa mvua hivyo wafanyabiashara wapeleke chakula kwenye maeneo hayo.

Waziri Mkuu amesema Serikali bado haijatoa kibali cha kutoa chakula nje ya nchi na kama kuna umuhimu kwa anayetaka anatakiwa akaombe ambapo kibali hicho kitahusu , kusaga kwaajili ya kusafirisha unga na siyo mahindi.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali imepokea barua za maombi ya kupeleka chakula nchi jirani, lakini bado haijatoa ruhusa na kuonya wale watakao kamatwa wakisafirisha mahindi nje ya nchi kinyume na utaratibu, mahindi hayo yatataifishwa na kupelekwa kwenye ghala la Taifa na magari yatapelekwa polisi

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments