Monday, June 26, 2017

Trump akosa kuandaa chakula cha Eid White House

Rais wa Marekani Donald Trump, amevunja tamaduni ya karibu miaka ishirini kwa kukosa kuandaa chakula cha jioni kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Hafla hiyo inayoandaliwa katika ikulu ya White House imekuwa ikifanyika kila mwaka kutoka kipindi cha Rais Bill Clinton.
Sherehe za Eid al-Fitr ndio mwisho wa mfungo wa Ramadan wakati waislamu hufunga
Awali Bwana Trump amelaumiwa kwa kutumia maneno makali dhidi ya waislamu ikiwemo kampeni ya kutaka uchunguzi kufanyiwa misikiti nchini Marekani.
Alisema katika taarifa: "Kwa niaba ya watu wa Marekani na Melania ninatuma heri njema kwa waislamu wakati wanaposherehekea Eid al-Fitr.

Chakula cha kwanza cha Eid kilichoandaliwa Ikulu ya White House kiliandaliwa na Rais Thomas Jefferson mwaka 1805 kwa ujumbe kutoka Tunisia.
Sherehe hizo zilifufuliwa tena na Hillary Clinton mwaka 1996 wakati akiwa mama wa kwanza wa taifa.
Hafla hiyo ilianza kufanywa kila mwaka tangu mwaka 1999 na kuhudhuriwa na viongozi wa kiislamu mashuhuri nchini Marekani.

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments