Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
wa Marekani Rex Tillerson anasema kuwa nchi za Ghuba ni lazima zilegeze
hatua yao dhidi ya Qatar ambayo inalaumiwa na majirani zake kwa kuunga
mkono Ugaidi.
Saudi Arabia, Muungano wa nchi za kiarabu, Misri na
Bahrain walikata uhusiano wa usafiri na wa kidiplomasia na Qatar siku ya
Jumatatu.Bwana Tillerson anasema kuwa hatua hiyo inasabisha kuwepo madhara ya kibinadamu.
Licha la kumsifu Emir wa Qatar kwa kupuza uungwaji mkono makundi ya kigaidi, Bwana Tillerson anasema mengi yanahitaji kufanywa.
Naye Rais Trump ameishutumu Qatar kwa kufadhili ugaidi na kuitaka ikome.Awali Raisi Trump alikuwa ameadika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar,na kudai kuwa alishiriki katika uamuzi uliochukuliwa na Saudi Arabia pamoja na nchi zingine.
Ndege za Qatar zilipigwa marufuku ya kutumia anga za baadhi ya majirani zake.Hatua hiyo ya ghafla
ilichukuliwa baada ya msukosuko ambao umedumu miaka kadha kati ya Qatar na majirani zake wa
Ghuba.
No comments:
Write comments