Monday, June 26, 2017

Gabo amzungumzia Kanumba na Wema Sepetu

Msanii wa Filamu Tanzania, Gabo amesema si kweli tasnia ya filamu imeshuka baada ya kifo cha Steven Kanumba.


Muigizaji huyo ameeleza kuwa watu wengi wanaamini kutokuwepo kwa Kanumba kumedhoofisha soko la filamu za bongo movies ambae aliweza  kuleta changamoto ambazo kwa sasa hazipo.

“Sio kweli industry ipo vile vile, kwani jamaa alikuwa analeta changamoto kwa wacheza sinema wengi sana hivyo baada ya kuondoka ule ushindani ukawa umeshuka, hicho ndio kitu ambacho wanakikosa,” Gabo ameiambia Bongo Dot Home ya Times FM na kuongeza kuwa
“Lakini mimi nisema waendelee kuwa na mapenzi ya dhati ila wasisite kutoa malalamiko yao na kukosoa pale ambapo wanahisi pameenda tofauti kwa sababu changamoto za watu pekee ndio zinabadilisha.Tunajua hapo tunakosea inabidi tufanye hivi, kwa hiyo  tunabadilika kutokana na mawazo ya watu,” amesema Gabo.
Katika hatua nyingine Gabo amemuelezea muigizaji Wema Sepetu ni mtu wa namna gani katika ufanyaji kazi hasa pale walipokuwa wakishoot filamu yake mpya ‘Kisogo’.
“Ni dada mmoja ambaye yupo na utaratibu wake, ukiufuata na kuusikiliza utafanya nae kazi vizuri sana na atakuwa yupo poa sana. Ukiwa nje ya huo utaratibu unaweza kumuona ni msumbufu na ukamuona kero kwenye kazi,” ameeleza Gabo.

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments