Barakah The Price ameamua kujibu mapigo baada ya Bright kuongea kuwa
hajui kuandika mistari na amekuwa akirudia rudia maneno katika nyimbo
zake
Akiongea kwenye E News ya EATV, Barakah amesema hawezi kuongelea
lolote kuhusiana na hilo kwa kuwa hataki kuendelea kumpa kiki msanii
mwenzake huyo ambaye alimshirikisha kwenye wimbo wa ‘Nitunzie’.
“Hiyo inaitwa unatafuta kiki kwa pikipiki, mimi siwezi kuongea
nitakuwa nachafua brand yangu ya Rock Star na unajua mimi nikiongea watu
wanazingatia sana, hivyo siwezi kuongelea watu kama hao katika
interview zangu,” amesema msanii huyo.
Barakah ameongeza kwa kudai kuwa hamfahamu msanii anayeitwa Bright kwa kuwa anafanya kazi na wasanii wengi chipukizi.
Thursday, June 22, 2017
Barakah The Prince: Sitaki kumpa mtu ‘kiki’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments